Saturday, November 14, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, akizungumza wakati wa mashindano ya Mbio za Baiskeli Shinyanga yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB chini ya kauli mbiu ya “Shinyanga Yetu, Damu Yetu”, Novemba 14, 2026. Picha na Elizabeth Cosmas
Baadhi ya washiriki wakichuana katika mashindano ya Mbio za Baiskeli Shinyanga yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB chini ya kaulimbiu ya “Shinyanga Yetu, Damu Yetu”, Novemba 14, 2026.
Mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kwa wanawake, Jolene Juma, akimaliza mashindano ya kilomita 76 kutoka Kambarage, Shinyanga Mjini hadi Tinde, katika mashindano ya Mbio za Baiskeli Shinyanga yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB, Novemba 14, 2026.
Baadhi ya washiriki wakichuana katika mashindano ya Mbio za Baiskeli Shinyanga yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB chini ya kaulimbiu ya “Shinyanga Yetu, Damu Yetu”, Novemba 14, 2026.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza wakati wa mashindano ya Mbio za Baiskeli Shinyanga yaliyoandaliwa na benki hiyo chini ya kaulimbiu ya “Shinyanga Yetu, Damu Yetu'.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi milioni 2 kwa mshindi wa kwanza wa mbio za baiskeli kilomita 150, Boniphace Ngwata, katika mashindano ya Mbio za Baiskeli Shinyanga yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB
Washindi wa mbio za baiskeli za kilomita 150 kutoka Shinyanga hadi Isaka Boniphace Ngwata (katikati), Paul Lomuria na Gerald Konda (kulia).
Washindi wa mbio za baiskeli waliokimbia umbali wa kilomita 76 kutoka Kambarage, Shinyanga Mjini hadi Tinde, Jolene Juma (katikati) Makhikiri Joseph (kushoto) na Sindano Makhirikiri (kulia).
Washindi wa mbio za baiskeli za kundi la vijana chipukizi waliozunguka mara 50 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Joel Dotto (katikati) Kisu cha Kimasai (kushoto) na David Jeremiah (kulia).
CRDB YAIBUA VIPAJI VYA BAISKELI SHINYANGA, WASHINDI WATWAA MILIONI ZA FEDHA
Na Elizabeth Cosmas - Shinyanga
Waendesha baiskeli kutoka Tanzania na nchi jirani za Afrika Mashariki wamechuana katika mashindano ya Mbio za Baiskeli Shinyanga yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB, ambapo washindi wamezawadiwa mamilioni ya fedha, huku mashindano hayo yakiambatana na zoezi la uchangiaji damu salama.
Mashindano hayo yaliyofanyika Novemba 14,2026 chini ya kaulimbiu ya “Shinyanga Yetu, Damu Yetu” yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, yakilenga kukuza mchezo wa baiskeli, kuibua vipaji vya vijana na kuhamasisha jamii kuchangia damu salama.
Akizungumza katika mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kudhamini mashindano hayo na kuunga mkono juhudi za kukuza vipaji vya vijana kupitia michezo.
Mtatiro, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, amesema Serikali ina dhamira ya kuyapanua mashindano hayo mwaka 2027 kwa kuwashirikisha waendesha baiskeli kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ili kuongeza ushindani, kufungua fursa za ajira na kuitangaza Shinyanga kimataifa.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, amesema benki hiyo inaendelea kutumia michezo kama sehemu ya utekelezaji wa dhamira yake ya kuchangia maendeleo ya jamii, kukuza vipaji vya vijana na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi kupitia sekta ya michezo.











0 Comments