TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA NCHINI (TAKUKURU)IMEANDAA HAFLA YA IFTAARI KWA WADAU MBALI MBALI MKOANI SHINYANGA.
19 March 2026
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imeandaa hafla ya Iftaar kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuimarisha mahusiano na ushirikiano katika mapambano dhidi ya rushwa
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga amesisitiza umuhimu wa wadau kushirikiana kwa karibu na taasisi hiyo ili kuziba mianya ya rushwa katika utoaji wa huduma.
Mkuu Wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro (akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mboni Mhita):*
AmesemaWananchi wanapoona mazingira ya utendekaji wa rushwa, wahakikishe wanatoa taarifa kwa mamlaka husika kwa wakati.”
MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA WAKILI JULIUS MTATIRO AKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO..
Hafla hiyo imeenda sambamba na utoaji wa misaada katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu, ikiwa ni sehemu ya kuonyesha utu na mshikamano wa kijamii.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakili julius Mtatiro akikabidhi Msaada katika moja ya kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu
FLORA MASALU.. SHINYANGA

0 Comments