MANISPAA YA KAHAMA YAKABIDHI SH2.16 BILIONI KWA VIKUNDI 96 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU, RC MHITA ATAKA MIKOPO HIYO IWE CHACHU YA UWEZESHAJI KIUCHUMI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akikabidhi mfano wa hundi ya Sh2,167,520,000 kwa ajili ya vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026. Picha na Kadama Malunde
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akikabidhi mfano wa hundi ya Sh2,167,520,000 kwa ajili ya vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026. 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya Sh2,167,520,000 kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya Sh2,167,520,000 kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.
Mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, Adam Mohamed Mlasi, akitoa neno la shukrani kwa Serikali na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kuwawezesha kupata mikopo kupitia mpango wa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, Novemba 5, 2026.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Francis Mlacha, akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo yenye thamani ya Sh2.16 bilioni kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Masudi Kibetu, akitoa taarifa ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, akieleza kiasi cha fedha kilichotolewa, idadi ya vikundi vilivyonufaika na mipango ya kuendelea kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Novemba 5, 2026.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Kahama, Thomas Muyonga, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo yenye thamani ya Sh2.16 bilioni kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Novemba 5, 2026.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Mataluma Kaniki, akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo ya Sh2.16 bilioni kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, akieleza dhamira ya Manispaa hiyo kuongeza mikopo hadi kufikia Sh4 bilioni ifikapo Juni 2027, Novemba 5, 2026.

Na Neema Nkumbi, Kahama

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imetoa mikopo yenye thamani ya Sh2,167,520,000 kwa vikundi 96 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, akitaka wanufaika waunganishwe na fursa za zabuni za Serikali ili kukuza biashara zao na kuongeza uwezo wa kurejesha mikopo hiyo.

Mikopo hiyo imetolewa Novemba 5, 2026, katika hafla ya utoaji wa mikopo iliyofanyika Manispaa ya Kahama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama cha Mapinduzi (CCM), madiwani pamoja na wanufaika.

Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa katika hafla hiyo, kati ya fedha hizo, Sh708,520,000 zimetolewa kwa vikundi 46 vya wanawake, Sh1,428,000,000 kwa vikundi 45 vya vijana, huku vikundi vitano vya watu wenye ulemavu vikipewa Sh31,000,000.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhita amesema mpango wa mikopo ya asilimia 10 ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kuwawezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi kwa kuwapatia mitaji isiyo na riba.

Amesema utoaji wa mikopo pekee hautoshi kuhakikisha wanufaika wanafanikiwa, hivyo ni muhimu Halmashauri kuhakikisha wanapata elimu ya ujasiriamali, ushauri wa kitaalamu na fursa za masoko zitakazosaidia kukuza biashara zao.

Amesisitiza kuwa wanufaika wanapaswa kuunganishwa na fursa za zabuni zinazotolewa na Halmashauri, ili waweze kushiriki katika uzalishaji wa bidhaa na utoaji wa huduma zinazohitajika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ametolea mfano vijana wanaoweza kuzalisha bidhaa na vifaa vinavyohitajika katika miradi ya Serikali, akieleza kuwa badala ya Halmashauri kununua bidhaa hizo kutoka kwa wazalishaji wa nje, ni vyema kuwapa kipaumbele wajasiriamali wa ndani ambao wamewezeshwa kupitia mikopo hiyo.

Kwa mujibu wa Mhita, utaratibu huo utawasaidia wanufaika kupata masoko ya uhakika, kuongeza kipato na kuimarisha uwezo wao wa kurejesha mikopo, sambamba na kujenga historia nzuri ya mikopo itakayowawezesha kupata mitaji mikubwa zaidi kutoka taasisi za fedha kama NMB na Azania Bank.

Aidha, amewataka viongozi wa Halmashauri na wataalamu wa maendeleo ya jamii kuhakikisha wanufaika wanapatiwa elimu ya usimamizi wa fedha, ujasiriamali na uendeshaji wa biashara ili kuhakikisha mikopo hiyo inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Amesema mafanikio ya mpango huo yanahitaji usimamizi na ufuatiliaji wa karibu wa miradi pamoja na urejeshaji wa mikopo kwa wakati, ili fedha hizo ziendelee kutumika kuwawezesha wananchi wengine.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Francis Mlacha, amewataka wanufaika kutumia fedha walizopatiwa kwa shughuli za kiuchumi walizoziainisha katika maombi yao badala ya kuelekeza mikopo hiyo kwenye matumizi mengine.

Amesema mikopo hiyo haina riba na inapaswa kuchukuliwa kama mbegu ya kujenga msingi wa kujitegemea kiuchumi

Post a Comment

0 Comments