
Na, Mwandishi Wetu -Nairobi , Kenya
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinaendelea na mkutano wao jijini Nairobi, Kenya, kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño zinazotarajiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Siku ya pili ya mkutano huo ulioanza Novemba 04, 2026, Maafisa Wakuu wa Usimamizi wa Maafa wa nchi wanachama wa EAC wamejadili mpango wa pamoja wa namna ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza katika Kanda.







0 Comments