MBUNGE WA JIMBO LA ITILIMA NJALU SILANGA ATEMBELEA VIJIJI SABA KATIKA KATA YA ITILIMA ATATUA KERO MBALIMBALI ZA WAKAZI WA ENEO HILO

 Mbunge wa Jimbo la Itilima, *Mhe. Njalú Daudi Silanga*, amesema ni wajibu wake kama mwakilishi wa wananchi kuwajuza hatua za utekelezaji wa ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni.

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe. Silanga amesema amefanikiwa kufanya mikutano katika vijiji saba ndani ya kata saba kwa lengo la kushukuru, kutoa taarifa  sambamba na kusikiliza kero za wananchi.

Katika ziara hiyo ametembelea vijiji vya Mhunze, Shishani, Ndoleleji, Ng'walali, Mwamakili na Kijiji cha Gaswa*.

Akizieleza sababu 3 kuu za ziara hiyo, Mbunge Silanga amesema:

Lengo Kuwashukuru wananchi wa Itilima kwa kura nyingi walizompigia wakati wa uchaguzi.

*Pili*: Kuwajuza utekelezaji wa ahadi na hatua zinazoendelea ili kuboresha huduma katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

*Tatu*: Kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Katika ziara hiyo amekuwa akiambatana na viongozi wa chama pamoja na wataalam kutoka sekta mbalimbali ambao ni sehemu ya utatuzi wa changamoto.

Mbunge huyo amewashukuru wananchi wa Itilima kwa mapokezi mazuri na mikutano yenye tija, akisema hiyo ni ishara ya kiu ya maendeleo iliyopo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Ziara ya Mbunge inatarajiwa kuendelea katika maeneo mengine ya jimbo la Itilima..

Mbunge wa jimbo la itilima  Njalu Silaga
 akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

Post a Comment

0 Comments