WATU SITA WAFARIKI NA 55 KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI SINGIDA


Watu sita wamepoteza maisha na wengine 55 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Greenline kupinduka katika Kijiji cha Mkiwa, Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Ajali hiyo imetokea wakati basi hilo lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea mkoani Mwanza likijaribu kukwepa shimo barabarani, jambo lililosababisha dereva kushindwa kulimudu chombo hicho na kupelekea maafa hayo.

Majeruhi wote 55 wamekimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya dharura, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika hospitali hiyo.

Jeshi la Polisi mkoani Singida limeanza uchunguzi wa kina wa tukio hilo huku likiwahimiza madereva kuchukua tahadhari wanapopita katika maeneo yenye changamoto za miundombinu ili kulinda usalama wa abiria na mali zao.

Post a Comment

0 Comments